BRUNO JULIAN: HISTORIA YAKE FUPI HII HAPA.

Wakati harakati za kampeni zikiwa zimepamba moto, nimefanikiwa kufanya mahojiano mafupi na mgombea urais wa shirikisho (Federal presidential post) chuo kikuu cha Dodoma. Bruno Julian ni nani?

Bruno Julian alizaliwa mwaka 1985 katika kijiji cha Iteera kilichoko katika wilaya ya Karagwe kwenye familia ya mzee Bruno Kayoza. Alianza masomo ya elimu ya msingi katika shule ya msingi Iteera mwaka 1995 na kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2001. Bruno alifaulu kujiunga na masomo ya elimu ya sekondari Shule ya sekondari ya Bugene mwaka 2002 na kuhimu kidato cha nne mwaka 2005 na akafaulu kujiunga na kidato cha tano na sita shule ya sekondari Tabora Boys mwaka 2006 hadi 2008.

Akiwa anaendelea na masomo yake shuleni Tabora Boys, Bruno Julian alikuwa akijihusisha na 'Scout services' akiwa kama kiongozi wa wacheza scout
shuleni hapo.

Baada ya kuhitimu kidato cha sita, Bruno Julian alijiunga na chuo cha ualimu kwa ngazi ya stashada Bunda mwaka 2008 hadi 2010. Alipohimitimu chuo cha ualimu, alifanya kazi kwenye makampuni anuai ikiwa ni pamoja na shirika la Msoma Utalii kwa miaka miwili mfululizo: 2010-2012, na wakati huo wakimpachika jina la Magufuli wa pili. Hatimaye aliamua kufanya kazi kama mwalimu Shule ya Sekondari Marya iliyoko wilaya ya Kwimba, mkoa wa Mwanza.

Bruno Julian, kama kiongozi wa scout, alishiriki mbio mbalimbali za mwenge mkoani mwanza.

Katika mahojiano mafupi niliyofanya naye katika chumba namba 73 block I leo tarehe 20 May, 2016 masaa machache kabla ya kuelekea kwenye kampeni zake katika viwanja vya COED, nilimhoji maswali mawili ya muhimu ambayo nilitaka kujua yeye kama yeye, anayazungumziaje katika kampeni zake na nini harakati zake katika kuyafuyatatua matatizo hayo.

Swali la kwanza lilikuwa ni je, suala la system ku-shake, ambalo limekuwa ni kero kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma, na wengi wamekuwa wakiacha masomo kwa suala kama hilo. Jibu lake lilikuwa ni kwamba, atakapokuwa rais; rais wa federal, atalifuatilia kwa wafanyakazi. "...suala hili kaka limekuwa likiwapotezea wanafunzi kwanza muda...lakini pia resources, kwa hiyo wanafunzi wanaumia..." alisema Bruno. '...pamoja na hayo kaka, ieleweke kuwa, ofisi ni mali ya umma...siyo unaenda ofisini unatukanwa, serikali haitaki watu wake wanyanyasike...' Aliendelea kukazia.

Swali langu la pili lilikuwa ni juu ya wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza wanapoanza masomo, kuuziwa vitabu kwa nambari ya usajili 'T/UDOM/ kwa lengo la  kuwashinikiza kununua. Katika kulijibu hilo, Bruno aliomba kuachana kwanza na suala hilo ili lisije kutengeneza mgogoro baina ya wahadhiri na wanafunzi. Amesema, '...suala hilo kaka sintolizungumzia...tuliache kama lilivyo...'. Lakini pamoja na hayo pia, ametoa wito kwa wanafunzi kujenga ukaribu wa manufaa na wahadhiri na wahudhurie vipindi kutokana na matakwa ya wahadhiri wao.

Swali lingine nililoliuliza mwisho kabisa lilikuwa ni miundo mbinu mibovu ya chuo kikuu cha Dodoma, hasa koleji ya Elimu. Bw. Bruno amesema, atatatua masuala ya miundo mbinu kupitia kwa marais wa vitivo na hivyo anaomba wapiga kura wawe makini kuwachagua marais wa vitivo walio 'shap' ili kurahisisha utoaji huduma kwa wanachuo.

Chapisha Maoni

0 Maoni