HATIMAYE BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU (HESLB) YAKUBALI KUREJESHA 8500 KWA SIKU

DAR ES SALAAM.
Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imekubali kurejesha kiasi cha shilingi 8500 kwa siku baada ya shinikizo la serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar Es Salaam.

Hapo awali, bodi hii ya  mikopo ilikuwa imeweka utaratibu mpya
wa kutoa pesa ya chakula kulingana na kiwango cha mikopo kwa asilimia alizopata mwanafunzi, halil ambayo ilisababisha wanafunzi wengi kupata hadi Sh 30 hadi 40 elfu kwa miezi miwili, badala ya sh laki 5 na 20. Awali suala hili lilizua sintofahamu ambayo ilikatisha tamaa wanafunzi wengi kuendelea na masomo.

Chapisha Maoni

0 Maoni