HII KALI: MWENYEKIT WA CCM MKOANI GEITA JOSEPH MSUKUMA AMVUA UKUU MKUU WA SHULE OTIENO SHULE YA SEKONDARI KASAMWA


Wiki iliyopita Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Maarufu kama Msukuma alimvua ukuu wa shule ya Sekondari Kasamwa bwana Denissi Otieno kwa kukataa kuwaruhusu wanafunzi wa CCM walioanzisha MAGUFULI CLUB chini ya mwalimu mwanaccm shuleni kinyume na sheria na kanuni Za utumishi wa umma
.

Wanafunzi wa CCM wanachama wa MAGUFULI CLUB shule ya Sekondari Kasamwa walikua na mahafali shuleni hapo maana walikua wanafanya siasa shuleni bila bughugha ingawa mkuu wa shule alikua akigombana Sana na Mwalim mlezi wa wanafunzi wa MAGUFULI club ambaye ni rafiki mkubwa Sana wa Msukuma na anatoka kijiji kimoja na Magufuli Chato.

Mkuu wa shule Denissi Otieno alifikia kikomo cha UVUMILIVU (Zero tolerance) baada ya Mwalim huyo mwanaccm kutangaza assemble kwamba kidato cha nne wote wanachama wa MAGUFULI club wavae nguo za Ccm kwa ajili ya mahafali ndipo Mkuu wa shule akagoma jambo Hilo kufanyika shuleni kinyume na kanuni na sheria za utumishi wa umma. Kanuni Za utumishi wa umma to leo la 2009 (public service standing order, 2009) kanuni namba F21 (a) - (h) inakataza kabisa mambo ya siasa kufanyika eneo la Kazi na Muda wa Kazi.

Pia sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 12(2) kimekataza kabisa shughuli za kisiasa kufanyika shuleni na taasisi nyingine za umma ikiwa ni Pamoja na kuanzisha tawi la chama, Umoja wa wanawake au Baraza La wanawake, vijana nk.

Mkuu wa shule alipokua anatangaza kupinga wanafunzi kufanyia mahafali shuleni, Mwalim mwanaccm aliirekodi speech ya mkuu wa shule na kumtumia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Bwana msukuma, usalama wa taifa, mkurugenzi mtendaji nk.

Msukuma aliamua kumvua uongozi wa ukuu wa shule Denissi Otieno na kuagiza afisa elimu na mkurugenzi kumpatia Barua mwalimu huyo bila kumuhamisha shule na kumpangia vipindi vya kufundisha.

CHANZO
jamiiforums

Chapisha Maoni

0 Maoni