Dr. Mashinji: Magufuli heshimu wataalamu na utaalamu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) *Dr. Vincent Mashinji* amepinga utenguzi wa aliyekuwa Mkurungenzi wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) Mwele Malecela kwa kuwa suala la utafiti ni swala la utaalamu na si swala la siasa.


Akiongea na waandishi habari mjini Iringa amesema kitaalamu utafiti hupigwa kwa utafiti na si kwa kumfukuza mtu kazi.

Mashinji anasema "Ili watu waweze kujikinga na magonjwa mbalimbali lazima tupate 'taarifa' za tafiti za wataalum zitakozotuwesha kutambua tatizo na kubaini ni njia zipi tutakazo zitumia kujikinga na magonjwa husika."

Pia amewataka wataalamu wa Tiba za binadamu na watafiti wote kutompa ushirikiano Mkurungezi mpya aliyeteuliwa ili kulinda heshima ya watafiti wote duiani na pia heshima ya taalum yao.

"Mh. Rais anatakiwa kuheshimu taaluma za watu ili kuwapa fursa wataalum waweze kufanyakazi kwa ufanisi," anasisitiza Mashinji.

Pia ametangaza ziara ya Kamati Kuu ya Chama hicho inayofanyika katika mikoa inayounda Kanda ya Nyasa

Ziara hiyo itaambatana na vikao vya ndani vyenye lengo la kuimarisha ujenzi wa chama kuanzia ngazi ya misingi, tawi, kata na itahitimishwa kwa uchaguzi wa kanda hiyo unaotarajiwa kufanyika Disemba 22.

Chapisha Maoni

0 Maoni