Hatimaye ile ndoa ambayo Bwana harusi aliishia mtini sasa yafungwa rasmi

Bwanaharusi Ndugu Samwel Makalobo akivishwa pete ya ndoa na Mke wake Given Mgaya katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya.Picha na Keneth Ngelesi . 
JamiiMojaBlog,Mbeya
HATIMAYE lile tukio lililovuta hisia za watu wengi la bibi harusi, Given Mgaya, kukimbiwa kanisani na mchumba wake siku ya harusi, limepatiwa jibu baada ya bwana harusi , Samwel Mwakalobo, kujirudi na kuamua kutimiza ahadi yake ya kufunga ndoa.
Ndoa hiyo imefungwa jana Desemba 23 majira ya saa tisa katika Kanisa la (K.K.K.T) Usharika wa Isanga na kufungishwa na Mchungaji, Mathias Andangile Mwakijungu, huku tukio hilo likishuhudiwa na idadi kubwa ya waumini na wananchi wa kawaida waliojitokeza kanisani hapo.
Kabla ya maharusi hao kula kiapo cha ndoa, Mchungaji Mwaijungu alitumia zaidi ya saa moja kutoa nasaha kwa maharusi kutokana na tukio lilotokea awali Disemba 16 mwaka huu baada ya Bwana harusi kuingia mitini bila kutoa sababu zozote.
Bwanaharusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23 mwaka huu. 
Bibi harusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23 mwaka huu. 

Mbali na kutoa nasaha kwa maharusi,pia Mchungaji Mwaijungu alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya waumini na watu wengine kuacha tabia ya kueleza mambo yasiyo yajua tena bila kuwa na uhakika.

Alisema tabia hiyo huenda ndiyo iliyosababisha tukio la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo baada ya baadhi waumini na watu wengine kwa maslai yao walimua kueleza uzushi ulio iibua taaruki kubwa.

Baada ya nasaha hizo na kunukukuu baadkitakatifu cha Bihi ya maandiko kutoka kitabu Biblia ndipo ulipo fika muda kwa maharusi hao kutimiza ahadi ya kula kiapo cha uaminifu katika ndoa yao.
Mara baada ya kufungisha ndoa hiyo nje ya kanisa hilo akizungumza na waandishi wa habari bwana harusi Mwakalobo alisema kuwa anawaomba radhi ndugu jamaa na marafiki na kwamba kilicho tokea ni mapito.

“ndugu zangu nawadhibitishia kuwa alipangelalo mungu binadamu hawezi kulitengua ni kwe;li tuliopnga tarehe ile lakini sisi ni wanadamu mungu alipanga huu ulikuwa ni upepo ulipita na niwaombe radhi ndugu jamaa kwa hili liliotokea” alisema Mwakalobo

Aidha katika hatua nyingine bibi harusi aligoma kuzungumzia suala hilo huku kwa kile alichokileza lile suala lililotokea kila kitu anamwachia Mungu.
 tabasamu la furaha la Bi Harusi baada ya kutoka kanisani 
Bwana na bibi harusi wakitoka kanisani.
Maharusi akitoka kanisani huku shwangwe zikitawala.

Chapisha Maoni

0 Maoni