Haya hapa mafanikio ya Izo Business mwaka huu 2016

Msanii wa Hip Hop kutoka Mbeya City Izzo Bussiness ambaye pia anafanya kazi na kundi la The Amazing linalofanya vizuri kwa sasa amefunguka na kusema miongoni mwa mafanikio aliyopata mwaka huu kutokana na muziki ni pamoja na kujenga nyumba.

Izzo Bussiness amekutana na kamera ya eNewz na kuzungumzia mafanikio aliyoyapata mwaka huu 2016 kupitia muziki wake ambapo amesema kuwa amefanikiwa ingawa siyo kwa asilimia 100 lakini amefanikiwa kwa asilimia 90 na anamshukuru Mungu.
Amesema katika mafanikio yake ameweza kujenga nyumba nyumbani kwao Mbeya na kuweza kuanzisha kundi la The Amazing ambalo mpaka sasa linafanya vizuri.
“Namshukuru Mungu nimeweza kutimiza malengo yangu mengi kwa mwaka huu katika kazi yangu na katika maisha yangu binafsi kwa ujumla nimeweza kufanya mengi nimeweza kujenga nimeweza kuanzisha kundi ambalo linafaya vizuri kwa sasa nashukuru na nimeanza na kujenga kwanza nyumbani halafu badaye nitajenga hapa Dar ni mipango tu”
Izzo Bussiness ni mmoja kati ya wasanii wa Hip Hop nchini ambao wameweza kufanya kazi nzuri na mwaka huu ameweza kutoa ngoma kupitia kundi la The Amazing ambalo yuko na mwanadada anayeitwa Bella Music.

Chapisha Maoni

0 Maoni