Hiki ndicho alichoongea Diamond kuhusu warembo Vera Sidika na Huddah

Mwimbaji wa Tanzania Diamond Platnumz leo December 24 2016 anafanya VODACOM WASAFI BEACH PARTY Jangwani Sea breeze ambapo miongoni mwa walioalikwa ni Warembo wawili maarufu kutoka Kenya, Vera Sidika na Huddah.

Kwa kitambo wawili hawa wameripotiwa kwamba hawako kwenye uhusiano mzuri yaani beef imetajwa kuwepo kati yao, Diamond ameulizwa kwenye Exclusive Interview na AyoTV kuhusu kuwakutanisha hawa wawili kwenye stage moja.
Platnumz amesema ‘Tuko katika kunogesha upendo na mimi siamini kama wana matatizo na sikuwa nafahamu‘ Full Interview ndio hii hapa chini unaweza kubonyeza play kumtazama Diamond


Chapisha Maoni

0 Maoni