Hivi ndivyo msanii Ali Kiba alivyokabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa soccer nchini Uganda.


Msanii Ali kiba akiwa na watu mashuhuri wengine walioshioriki katika mechi hiyo ya mfuko wakuchangia wakina mama wajawazito wajifungue salama wakiwa na kikombe chao baada ya kushinda mchezo huo wa hisani, wa pili ktoka kulia Dora Mwina Mwanzilishi wa Taasisi ya Dora Mwina Foundation.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo fleva' Alli Saleh Kiba "Ali Kiba" amecheza mechi ya kirafiki nchini Uganda na kufanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo iliyomshirikisha pia Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Ynaga Emanuel Okwi anayekipiga nchini Denmark.
"A celebrity For Charity Match" kama inavyojulikana, kwa mwaka huu taasisi ya Dorah Mwima Foundation ilimualika Ali Kiba kushiriki nao pamoja na kucheza mchezo huo wa kirafiki ikiwa na malengo ya kuchangia kwa hisani katika mfuko wa akina mama wajawazito kuweza kujifungua salama.Mchezo huo uliochezwa leo kwenye Viwanja vya Kabira Country Club umeambatana na burudani ya muziki kutoka kwa msanii huyo kutoka Tanzania huku ikiwa ni mara ya tatu kufanyika kwa tamasha hili linalojulikana kama Launching of the Mama Port Project

Mwanzilishi wa Taasisi ya Dora Mwina Foundation, Dora Mwina akisalimiana na msanii Ali kiba kabla ya mechi kuanza.
Msanii Ali kiba akiwa na kikombe chake alichokabidhiwa baada ya mechi kumalizika akizawadia kama nyota wa mechi hiyo akiisaidia timu yake kushinda kwa kufunga goli moja kati ya mawili.

Msanii Ali kiba akiwa na shambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga Emanuel Okwi anayekipiga nchini Denmark.

Chapisha Maoni

0 Maoni