Mtoto adaiwa kumuua baba yake huko Serengeti

Serengeti. Mkazi wa Kijiji cha Mesaga Kata ya Kenyamonta, Monyi Gasusu (53) anadaiwa kuuawa kwa kukatwa na panga na mtoto wake baada ya kumwambia akachunge mifugo.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi alisema kabla ya kufanya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa anamenya mihogo.

Kamanda alieleza zaidi kuwa,  Gasusu (marehemu) akamwambia mke wa mtoto wake  akachunge mifugo lakini naye akakataa  ndipo  akachukua  fimbo amchape.

Alisema kabla hajatimiza azma hiyo, mtuhumiwa alimuwahi kwa kumkataka kwa panga.

“Inaonekana kulikuwa na mgogoro kati yao maana kijana alikuwa ameshaambiwa

ahame hapo nyumbani kutokana na kutowatii mzazi wao,” alisema Kamanda Ng’hazi

Chapisha Maoni

0 Maoni