TAARIFA YA POLISI: Aliyetimuliwa Msumbiji afariki dunia njiani, aacha mtoto


Kuhusu ndugu wa marehemu, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, George Salala alisema ndugu zake bado hawajajitokeza na wanaendelea kuwasiliana na madaktari kujua chanzo cha kifo na Jackline. Alisema hadi juzi zaidi ya Watanzania 2,000 walikuwa wamerudi nchini.

Jackline Grayson, ambaye amefariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Ligula baada ya kurudishwa nchini kutoka Msumbuji, anadaiwa kuwa na wadogo zake wawili wanaoishi Ubungo Maziwa, Dar es Salaam na kwamba ni mwenyeji wa Njombe.

“Msumbiji alikuwa anafahamika kwa jina la Jackline Grayson, lakini nimesikia jina la nyumbani kwao ni Josephine Sanga. Dar es Salaam ana wadogo zake wawili ni vyema kama wakisikia taarifa hizi (wajitokeze),” alisema Agnes John ambaye anatunza mtoto wa marehemu.

Akiwa anajipanga kuanza upya maisha, Agnes, mmoja wa Watanzania waliotimuliwa Msumbiji, anakabiliwa na mambo mawili mazito; kumpoteza rafiki yake na kusaka ndugu wa mtoto wa mwaka mmoja aliyeachiwa.

Agnes, ambaye ni mwenyeji wa Mbeya, anaishi na Watanzania wengine waliorejeshwa nchini katika mahema yaliyowekwa Uwanja wa Mashujaa mjini hapa kusubiri kupiga hatua nyingine baada ya harakati zao za kutafuta maisha Msumbiji kukatishwa ghafla.

“Siwafahamu ndugu wa marehemu,” alisema Agnes na kuongeza: “Naomba ndugu zake wajitokeze ili kumzika na kufanya uamuzi kuhusu mtoto wake

Chapisha Maoni

0 Maoni