Kenyatta, Odinga Wakutana Uso kwa Uso Wafanya Mazungumzo ya Siri

Kenyatta, Odinga Wakutana  Uso kwa Uso  Wafanya Mazungumzo ya Siri
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amekutana na Kiongozi Mkuu wa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini humo, Raila Odinga na kufanya mazungumzo ya siri.

Wawili hao wamekutana leo Machi 09, 2018 na kufanya mazungumzo yao Ikulu jijini Nairobi ikiwa ni masaa machache tangu aingie nchini humo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson.

Bado haijajulikana ni jambo gani wameongea wawili hao ambao ndiyo walikuwa wagombea urais wenye nguvu kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2017.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimedai kuwa kwenye mazungumzo hayo huenda wakagusia masuala ya kisiasa ambayo bado ni gumzo na tishio la usalama nchini humo.

Hata hivyo, Leo Rais Kenyatta baada ya mazungumzo hayo amepanga kuongea na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza mazungumzo yake na Raila Odinga. 

Chapisha Maoni

0 Maoni