Moto wateketeza wanne wa familia moja

Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea moto.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Magwira, Kata ya Bwilingu wilayani Chalinze usiku wa kuamkia leo Machi 11,2018.

Chanzo cha moto hakijajulikana ingawa imeelezwa kulikuwa na tatizo la umeme kuzima na kuwaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amethibitisha tukio hilo akiahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

Chapisha Maoni

0 Maoni