Naibu Gavana Benki kuu asimulia walivyouziwa dhahabu bandia

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Bernard Y. Kibesse ameweka wazi kuwa iliacha kununua dhabu kwakuwa waliuziwa dhahabu feki.

Dkt. Kibesse aliyasema hayo jana Jijini Dar es salaam, katika Mkutano wa wachimbaji,  Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini.

Awali kabla ya kujibu  swali la Rais Magufuli ambaye aliuliza BOT imejipangaje licha ya kuwa hapo nyuma ilikuwa ikishirikiana na wauzaji wanaoibia serikali.

Dkt. Kibese alisema kwamba Benki Kuu haina tatizo na kununua dhahabu, hapo awali mpaka mwaka 1994 BoT ilikuwa ikinunua dhahabu, "taifa lenye watu wasio waaminifu, haliwezi kuwa Taifa endelevu, kilichotukuta tuliuziwa dhahabu feki tukaamua kusimamisha ununuzi".

"Tunafahamu kuwa 'Reserve' za Benki Kuu nyingi duniani zinakuwa na hazina za dola na dhahabu, nasi tunaweza lakini tupo tayari kuanza kununua tena. Tunaelewa Benki Kuu nyingi zinakuwa na hazina ya dhahabu.

“Tuko tayari kununua dhahabu ambayo tayari iko ‘refined’ (chakatwa) kwa sababu ndiyo kiwango ambacho kinakubalika kimataifa na nimefurahi kusikia kuwa kuna watu wana mitambo ya kufanya hivyo.

“Benki kuu tumeandaa sehemu ya kuhifadhi madini ndani ya utaratibu maalumu ambazo tutakubaliana kuwa ni lazima dhahabu inayokuwa pale iwe na mpangilio wake wa uhifadhiwaji.

“Kwa mfano mnunuzi hajapatikana hiyo dhahabu hairuhusiwi kukaa hapo zaidi ya siku tano na badala yake ipelekwe Center’.”  Alisema

Chapisha Maoni

0 Maoni