KICHEKESHO CHA LEO. SOMA HAPA UONGEZE SIKU ZA KUISHI

Mwalimu wa historia alikuwa anafundisha wanafunzi wa kidato cha kwanza mada ya AFRICAN RESISTANCE ANGAINST THE IMPOSITION OF COLONIAL RULE. Katika utangulizi wa mada hiyo, mwalimu alianza kwa kuuliza swali kwa wanafunzi, swali lilikuwa hivi: ni nani alimuua mtemi Mkwawa? Mwanafunzi wa kwanza akasema,"...mwalimu kiukweli mimi jana sikuwepo shuleni, mimi sijui...". Wa pili pia akasema, "...mwalimu mimi sijamuua kabisa mtemi Mkwawa...". Wanafunzi wote wakakana kuhusika na kifo cha mtemi.

Kwa kuona kuwa wanafunzi ni majuha, akaamua kumfuata mkuu wa shule ili aje kuona vile wanafunzi walivyo majuha.

Mkuu wa shule alipokuja, akauliza tena swali lile kwa mkwara mzito, "...nauliza kwa mara ya mwisho, ni nani alilyemuuza mtemi Mkwawa?". Basi wanafunzi wakaendelea kukana na wengine kutokana na mkwara wa mkuu wa shule wakaanza kulia. Mkuu wa shule alipoona kuwa hapati jibu, akamnong'oneza mwalimu mwenye somo,"...hivi una uhakika kuwa muuaji yumo kwenye hili darasa?..."

Mwalimu akaangua kicheko hatare....

Chapisha Maoni

0 Maoni