Labda tu nianze kwa kuseme kwamba, yapo mengi ya kukosea, na ni kawaida kukosea kwenye mambo hayo mengi, lakini hakuna kitu kibaya kama kurudia kurejesha kosa hilo kwenye mfumo wako wa maisha. Uongozi unaomalizia muda wake wa madaraka katika chuo kikuu cha Dodoma, hasa koleji ya Elimu (COED) ni uongozi uliokuwa na madhaifu mengi na ni mengi hasa. Kuna kero kadha wa kadha zimekuwa zikilalamikiwa na jamii ya wasomi katika chuo hiki, lakini hakuna kiongozi wa UDOSO ambaye amekuwa akijaribu kuchukua hatua za kukabiliana na kero hizo. Sasa filimbi imeshapulizwa, na wanasiasa wameshachukua fomu zao na sasa wapo kwenye kampeni tayari kujinadi kupewa kura na kuaminiwa kwa wapiga kura wao.
Mada yangu ya leo ni kuhusu kurudisha mfumo uleule ambao umekuwa ukipigiwa kerere muda mrefu sasa, ambao umekuwa mfumo wa viongozi wasiotaka kuwa
karibu na wapiga kura wao, ila wamekuwa wakijifungia tu ndani na madaraka yao kuoneka wakati wa kusaini boom, kwani hapo ndipo wamekuwa wakionesha utumishi wao kuwa ni wachapa kazi kwa kusimama mlangoni kwa ajili ya kudai risiti za UDOSO na kama haujawalipa, siku hiyo boom watahakikisha hautasaini, niliwahi kuuliza, hivi mnaponizuia kusaini, hiyo hela mtakuja kuilipa ninyi? Nilionekana anti-UDOSO na sikutaka kuwa na makuu; huu ndio uongozi unaomaliza muda wake hapa Dodoam, koleji ya Elimu.
Mada yangu ya leo ni mgombea mmoja wa urais wa koleji Bw. Mvungi Kombo, kama unavyomuona hapo pichani, ambaye pia alikuwa mbunge kwenye uongozi unaomaliza muda wake. Namkumbuka mvungi kwa jambo kubwa moja. Kipindi mwaka wa kwanza tunafanya udahili-awali kabisa wakati ndiyo tunafika hapa chuoni-Bwana Mvungi aliwahi kutukana wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa kusema, '...first year [mwaka wa kwanza] acheni ujinga na utoto, pangeni mstari..'. Huyu ndiye Mvungi Kombo ambaye leo anapita kwa hao hao wanafunzi mwaka wa kwanza kuwaomba kura, hivi ni kweli kwamba amesahau alivyowatusi bila kujali kama kuna mwaka wa kwanza waliokuwa wanamzidi umri; wengine umri sawa na baba yake? Ni sharau ya namna gani kwa kiongozi wa umma kama huyu, tena kwenye jamii ya wasomi kama hii kujiona yeye ni bora zaidi na kuwarushia matusi kadri alivyojisikia wanafunzi wa mwaka wa kwanza, leo hii ana nini kipya cha kutueleza? Ubunge tu ulimpa JEURI, vipi URAIS?
Kashfa ya pili ya Kombo ni hii hapa. Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika zinazosambaa kwenye makundi ya whatsapp, Mvungi alipokuwa mbunge aliwahi kupinga maslahi ya wawakilishi wa madarasa CRs baada ya kuwasilishwa kwa hoja kwamba, wawakilishi hao walitakiwa kulipwa, kwani wanafanya kazi kubwa kuliko hata mbuge; KOMBO alipinga vikali sana hoja hiyo. Cha kushangaza hadi hatua hii inafikia ya kupiga kura, hajawahi kuwataka radhi CRs na badoo naye anajiita MTU WA WATU, kwa kweli Kombo hastahili kiatu anachotaka kukinunua!
Walimu-wanafunzi wenzangu, kwa dharau za namna hii kwenye jamii kama hii ya kisomi, hazistahili kabisa na ni dhahiri, shahiri kabisa kuwa, hata akija kuwa rais, ipo siku atatutemea hata kohozi, kiongozi wa namna hii hatufai hata kidogo! Ni maoni tu.
1 Maoni
mfanye kwel kwenye kupgia kura
JibuFutaTUANDIKIE MAONI YAKO HAPA