Tanga.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amealikwa kuhudhuria
mkutano mkuu wa Oktoba 29, utakaowajadili madiwani wa chama hicho
kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga waliopigana kwenye kikao cha kamati
ya utendaji.
Akizungumza ofisini kwake juzi, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga,
Rashid Jumbe alisema madiwani hao na mbunge watajadiliwa na mkutano
mkuu utakaoongozwa na Maalim Seif, utakaoamua hatima ya mgogoro huo.
Jumbe alisema mkutano huo utakuwa na ajenda mbili; hatima ya mgogoro wa
umeya wa Jiji la Tanga na nidhamu ambayo itawahusu madiwani 11 na
Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruk.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA