Arusha: Yaliyojiri kutoka mahakamani Arusha, dhamana ya Mbunge Lema yashindikana

Baada ya Mahakama kuu kanda ya Arusha kutupilia mbali maombi ya mawakili wa Lema ya kufanya marejeo ya hukumu ya dhamana. Na Mawakili wa Lema kukata Rufaa kwa hati ya dharura kesi hiyo itaanza kusikilizwa tena kuanzia leo siku ya jumatatu Mbele ya Jaji Massengi, Jaji Mwandamizi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Wakili wake, Peter Kibatala amesema walikata rufaa chini ya hati ya dharura kuomba Mahakama isikilize kesi hiyo mapema.

Amesema waliamua kufuata maelekezo ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Mosha ya kuwataka kukata rufaa.

Katibu wa mbunge huyo, Innocent Kisanyage amesema rufaa hiyo itasikilizwa leo saa tatu asubuhi baada ya kukamilisha mambo yanayotakiwa.

Taarifa ambazo tumezipata Mbunge Godbless Lema atafikishwa ndani eneo la mahakama kuanzia saa tatu asubuhi.

Maskari waliovaa kininja na silaha za kali za moto wametapakaa kila sehemu.

Mbunge Godbless Lema ameshafikishwa katika viwanja vya mahakamani.
Mbunge Godbless Lema atapandishwa kizimbani majira ya saa sita.
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro Mbunge wa Jimbo la Monduli Julias Kalanga wameshawasili tayari mahakamani .
Jaji bado hajafika.
Hatma ya Lema kujulikana leo, Bado hajapandishwa kizimbani.

KESI YAAHIRISHWA: Mahakama Kuu Arusha yamnyima dhamana Mbunge Lema; mawakili walipaswa kupeleka notisi ya rufaa kwanza na siyo kukata rufaa; arudishwa rumande hadi Desemba 2.

========

Rufaa ya mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema iliyopangwa kutolewa leo imeshindikana baada upande wa Jamhuri kuweka pingamizi ya kuwasilisha notisi badala ya rufaa, ambapo Mbunge huyo amerudishwa rumande kwa ya mara tatu.

Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J Marandu ambaye amesema wamefanya hivyo ili kuharakisha na wamekubaliana na pande zote mbili.

Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wameshakamilisha taratibu za kisheria kuhusiana na pingamizi hilo na wanasubiri pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.

Jaji aliyekuwa akisikiliza pingamizi hilo Fatma Masengi ameelekeza upande wa serikali wawasilishe hoja zao kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.

Chapisha Maoni

0 Maoni