TAHLISO YAWATAKA WANAFUNZI WOTE ELIMU YA JUU KUTOKUJAZA DODOSO LA HESLB

Chama cha marais vyuo vikuu Tanzania TAHLISO wametoa tamko la pamoja kuwataka wanafunzi wote wa elimu ya juu kutokujaza dodoso la bodi ya mikopo hadi pale watakapojiridhisha kuwa halitakuwa na madhara kwa wanafunzi.


Akiongea kwa njia ya simu moja kwa moja na bloga kwa niaba ya chama hicho, rais wa shirikisho chuo kikuu cha Dodoma, Bw. Bruno Julian Kayoza amesema, kwa sasa wanafunzi wanatakiwa kuwa watulivu na kusubiri hadi pale tamko jipya litakapotolewa na chuma hicho."...

Aidha, Bw. Bruno ametaja sababu ya kuwataka wanafunzi kutokulijaza dodoso hilo kuwa, wanafunzi wote walishajaza taarifa zote muhimu wakati wakiomba mkopo."...hatujaona maana ya dodoso hilo, maana kama taarifa muhimu, wanafunzi wote walishajaza, sasa ni kama usumbufu..." Amesema.

Sanjari na hilo, chama hicho kimekubaliana kukutana tarehe 5 Novemba ambapo kinatarajia kuwa na mazungumzo na waziri wa elimu, sayansi na teknoloji Prof. Ndalichako pamoja na mkurugenzi wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu HESLB.

Chapisha Maoni

0 Maoni