Chuo cha kimataifa kujengwa Mbeya


Chuo cha kimataifa cha marubani nchini kinatarajiwa kujengwa katika kiwanja kidogo cha ndege kilichopo katikati ya jiji la Mbeya.


Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Laurent Mwigune ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, wananchi na viongozi wa TAA.
Awali, mkazi wa Kata ya Iyela, John Mwanguku alilalamikia eneo hilo kuwa ni la wazazi wao tangu mwaka 1977 na kwamba walikubaliana na wataalamu kuwapimia viwanja vya makazi vyenye hati miliki ili waviendeleze.
Aidha Mwanguku alisema walikubaliana na maofisa ardhi waifanye kazi ya kupima viwanja kwa maelewano ya kupewa viwanja 10 kati ya vitakavyopatikana ndani ya uwanja huo wa ndege.
Hata hivyo, Mwigune amesema uwanja wote wa ndege utaendelea kumilikiwa na Taa, pia wana mipango ya kujenga chuo cha kimataifa kufundishia marubani.
“Tumeshtushwa kupata taarifa za ugawaji wa viwanja kinyemela kwa kuwa uwanja huu bado uko mikononi mwetu, tunatarajia kujenga chuo cha kimataifa cha marubani ili kuiwezesha nchi kuwa na marubani wa kutosha,” alisema Mwigune.
BY: EMMY MWAIPOPO
CHANZO: MWANANCHI

Chapisha Maoni

0 Maoni