JONAS MKUDE: Kinachowaangamiza Simba ni kiburi, Jifunzeni kutokana na haya.

Inasemekana kwamba jitihada za Jonas Mkude kuongeza mkataba na klabu yake Simba SC upo kwenye utata mkubwa sana.

Inaonekana mkataba mpya wa Jonas Mkude unadai alipwe fedha zaidi ambazo amekuwa akilipwa kipindi aongezapo mkataba.

Hili suala la ongezeko la pesa za kusaini mkataba mpya limefanya viongozi wa simba sc kumuona kama mchezaji huyo ni msaliti na kuwa hana mapenzi na timu hiyo ambayo imemlea tangu ujana wake.

Hanspope alionekana kulalamika kwenye moja ya chombo cha Habari kuwa haiwezekani mchezaji waliomlea na kumkuza wao wenyewe atake kiasi kikubwa cha pesa ili aongeze mkataba.

"Kama ataki kucheza simba basi aende huko Yanga SC ambapo watamlipa hizo pesa... Mchezaji amejaa tamaa ya pesa sana" Alisema Hans Pope

.................................................................................

Simba ndio mnao haribu soka la Bongo. Mnasindwa kujua kuwa sasa ni wakati wa kubadilisha soka kutoka la Burudani kuwa la kulipwa..

Kumbukeni kuwa hawa vijana hawana kazi, wameamua kufanya soka kuwa ni kazi. Inapaswa kazi yao iheshimiwe kama kazi yako wewe inavyoheshimika....

Yule ni mchezaji wa kumtegemea sana kwenye kikosi chenu kwa sasa (zaidi ya kichuya) cha kushangaza mnamchukulia kama kapuku fulani hivi... Yaani iweje Mavugo alipwe pesa ndefu zaidi yake.. Ukizingatia yeye ndiyo mwenye kiwango zaidi ya huyo Mavugo.

Igeni waingereza pale. Ona salary ya Rooney! Kipindi anafanyiwa salary increment yeye ndiye alikuwa dependable player.

Huwa mnajifanya viburi sana. Eti ohh acha aende simba ni kubwa kuliko yeye. Hilo si sawa kabisa.

Inaonekana bado hamjajifunza mpaka leo.

1. Tangu Yondani asepe hamkuwahi pata mlinzi mwenye hadhi yake....

2. Tangu Tambwe asepe hamjawahi pata striker mwenye hadhi yake na ubora wake.

3. Tangu Messi "Singano" asepe hamjawahi pata winga wa kulia mwenye uwezo kama yeye (licha ya kuwa Kichuya anajaribu kuwasahaulisha....

4. Tangu Kessy asepe hamjafanikiwa kumpata mbadala wa huyu kijana. (Mnatudanganya kuwa Bokungu ameweza)

5. Tangu akina Barthez na Dida wasepe pale hamjawahi pata walinda milango wenye ubora sawa na wakudumu kwa kitambo kirefu.... 

Simba acheni kiburi cha kujiona kuwa mnauwezo wa kuwaacha wachezaji wenu muhimu na kujidai kuwa mna uwezo mzuri wa kuwa replace.

Chapisha Maoni

0 Maoni