Msafara wa ndege za ajabu wawasili nchini

Msafara unaovutia macho ya watu wengi duniani wa ndege za zamani, ambao umeanzia nchini Ugiriki na kumalizikia nchini Afrika Kusini umewasili nchini katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.


Baadhi ya marubani wa msafara wa ndege za kale (Vintage) wakiwa mbele ya moja ya ndege hizo baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar

Msafara huo unahusisha ndege zenye umri wa zaidi ya miaka tisini huku Tanzania ikiwa ni moja kati ya nchi nane za Afrika ambako msafara huo unapitia.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt. Miraji Ukuti Ussi ameomba Zanzibar iwe mwenyeji na muandaaji wa tukio la kitalii la msafara wa ndege hizo za kizamani linalofanyika kila mwaka.

Amesema kwamba Zanzibar ina uwezo wa kufanya hivyo kwani hiyo ni fursa itakayoongeza idadi ya watalii wanaoitembelea Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Kwa upande wao, waandaaji wa msafara huo wamesema ni heshima na fursa kubwa ya kiuchumi kwa Tanzania, kwani kwa muda wa siku tano ambazo msafara huo upo nchini, dunia inaiangalia Tanzania na kuitangaza kiutalii huku idadi kubwa ya watalii wakiwa wamewasili kushuhudia moja ya matukio adimu kufanyika duniani hivi sasa.

Chapisha Maoni

0 Maoni