Mwanafunzi kidato cha tatu anusurika kufa baada ya kubakwa na kutelekezwa kwenye korongo

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo
Na Woinde Shizza,Meru

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo
Meru  mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na kuteketezwa


kwenye  korongo la mchanga na kusababishiwa  maumivu makali
yaliyomsababishia kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.

Akielezea tukio hilo  mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za
kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa 12.30
alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo
aliyemfanyia kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili
asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili ambacho
kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.

"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba
shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimejipelekea nishindwe
kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo nimeonekana aliniumiza
sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu"alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli
Akyoo  alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti
zao ni vema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani
tangu akamatwe mtuhumiw huyo na kupellekwa kituoni bado hajasomewa shtaka
linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na vitendo hivyo kuona wako sawa
kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo

Nae mkuu wa shule hiyo Nkoe Nicolaus  alisema kuwa tukio hilo limemfanya
mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili huo
ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri wazazi wa
binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia nyingine ili kimbadilisha
mawazo ya kifkra.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesco Samweli Matayo
alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa mara
baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa aliyetambulika kwa
jina la Wilson  Elias ambae ndie  aliyehusika na ukatili huo  na kumfikisha
katika kituo kidogo cha polisi usa river ili kukabiliana na shutuma hizo.

Kamanda wa  polisi  Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo ambapo limesema
kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016  na atafikishwa
mahamani upelelezi ukikamilika.

Chapisha Maoni

0 Maoni