ZITTO amtembelea Lema gerezani, amwambia siku zote haki hushinda.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa mara nyingine leo (jana) amenyimwa dhamana na imeamriwa na mahakama kuwa akae mahabusu mpaka Februari mwakani kesi yake itakapotajwa tena.


Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya kuridhishwa na vigezo vya kisheria ambavyo vilitolewa na mawakili wa Jamhuri ambao waliweka pingamizi Lema asipewe dhamana.

Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), alimtembelea Lema gerezani leo na haya ndiyo ameyaandika kuhusu Lema, kesi yake na hali ya kunyimwa dhamana.

ZITTO KABWE:

Leo (jana) Ijumaa Desemba 2/2016 nimepata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza la Kuvu la Arusha. Nimemtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati za kutafuta na kulinda haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa sana na ukiukwaji mkubwa wa haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona ni bora akae ndani mpaka hapo dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana.

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.

Amemshukuru Mungu Kwa kumpa mke jasiri anayempa moyo na ndio ngome yake kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka haki kutendeka katika uendeshaji wa nchi yetu. Siku zote haki hushinda.

Chapisha Maoni

0 Maoni