Muungano wa Afrika umekuwa ukihimiza mataifa wanachama wajitoe ICC
Hatua ya taifa la Afrika kusini kujiondoa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefutiliwa mbali na mahakama nchini humo iliyosema kuwa uamuzi huo ni kinyume na katiba na haufai.
Afrika Kusini iliarifu Umoja wa Mataifa kuhusu lengo lake la kutaka kujiondoa, ikiishtumu mahakama hiyo kwa kukandamiza uhuru wake.
Lakini chama cha upinzani cha Democratic Alliance DA kilisema kuwa serikali lazima itafute uungwaji mkono bungeni.
Mahakama hiyo iliagiza serikali kufutilia mbali notisi yake ya kutaka kujiondoa.
Uamuzi wa wa kutakankujiondoa ulijiri kufuatia mgogoro kuhusu ziara ya rais wa Sudan Omar al Bashir nchini humo 2015.
Mamlaka ya Afrika Kusini ilikataa kumkamata BwBashir licha ya kuwa amewekewa agizo la kukamatwa na mahakama hiyo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA