Habari njema kutoka CCM Urambo, Tabora

UONGOZI wa Chama Chama Minduzi (CCM) Wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora umesema kuwa umeshaanza mikakati ya kuongeza vyanzo vya mapato kwa kuanza kuviratibu viwanja vyake vyote.

Akizungumza ofisini kwake Mei 17, Katibu wa chama hicho Latifa Malimi alisema kuwa mbali ya uwanja huo wa michezo, pia kwenye jengo la ofisi kuna maeneo ambayo uongozi uliopita ulishaanza zoezi la kuyapatia hati nao wameshalifikisha katika hatua nzuri na kwamba lengo ni uboreshaji wa vyanzo vya mapato.

Alieleza kuwa upande wa uwanja wa michezo wa Mirambo, mwezi Machi wameshaanza zoezi la upatikanaji wa hati na kuwa wapo katika hatu nzuri, huku akieleza baada ya kukamilishwa kwa zoezi hilo wataitisha kikao kitachohusisha wadau lengo kuuboresha zaidi na hatimae kutumika kwa michezo mbalimbali sanjali na Ligi ngazi zote.

"Tunaboresha vyanzo vya kiuchumi, hapa eneo la jengo la ofisi tuna viwanja ambavyo tayari tushapata hati zake, sasa tunafuatilia hati ya uwanja wetu wa Mirambo, mchakato unakwenda vizuri, tukikamilisha hilo tutaitisha kikao cha wadau tuweze kupanga mikakati ya kuuboresha zaidi uweze kutumika kwa michezo yote ikiwemo Ligi tofauti," alisema Latifa.

"Tumekuwa wamiliki wa uwanja wa Mpira wa Miguu wa Mirambo, hivi sasa kilichopo ni ufuatiliaji hati tu ambayo wenzetu walikuwepo wameshaanza zoezi hilo, nasi tuna3nf3lea nalo vizuri, natoa wito kwa wananchi waendelee kuutumia uwanja wao," aalisema Latifa.

Alimalizia kwa kusema kwamba sera ya chqma hicho pia inagusa michezo, hivyo kwa kutumia uwanja huo watakuwa wanatekeleza kikamilifu ilani ya chama kwa kuwapatia fursa vijana  na watu wa rika mbalimbali kuweza kuutumia uwanja huo.

"CCM sera yake inagusa pia sekta ya michezo, nitumie fursa hii kiwaeleza wana-Urambo kwamba uwanja ule ni wao, sisi viongozi tutaitisha kikaona wadau wa michezo wakiwemo wao ili kwa umoja wetu tuchangiane mawazo ya namna ya kuufanya uwe wa kisasa kama ilivyo kwa baadhi ya viwanja vya wilaya nyingine hapa nchini," alimalizia Katibu huyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni