Huyu ndiye Peter Munk, Mwanzilishi wa Barrick Gold Corporation, mmiliki wa zaidi ya asilimia 60 za Acacia


Peter Munk (83), Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Barrick Gold Corporation, kampuni inayomiliki zaidi ya asilimia 60 ya Hisa za Acacia.

Alizaliwa November 8, 1927, Ni raia wa Canada, mfanyabiashara na mtoa misaada mashuhuri zaidi duniani . Munk ndie Mwanzilishi na Mwenyekiti wa kampuni kubwa zaidi ya madini duniani ya Barrick Gold Corporation .

Munk alizaliwa katika mji wa Budapest, Hungary, katika familia ya kitajiri ya Wayahudi, kijana wa Katherine (Adler) and Louis L. Munk. Baada ya Hungary kuvamiwa na utawala wa Nazi wa Ujerumani chini ya Adolp Hittler mnamo Machi ,1944 Peter Munk alikuwa kijana mdogo wa umri usiozidi Miaka ishirini. Familia yake ilitoroka kupitia treni ya Kastner , Treni ambyo ilibeba wayahudi takribani 1,684 na kuwapeleka nchini Switzerland, mpango ulioratibiwa na Rudolf Kastner, Mhafidhina wa taasisi iliyojulikana kama Zionist Aid and Rescue Committee .

Taasisi hii ilitumika kuwatorosha Wayahudi kutoka Hungary kufuatia majadiliano na Afisa wa ngazi za Juu ya Ulinzi wa Hungary Adolf Eichmann kwa kubadilishana fedha, dhahabu, almasi kwa kile kilichojulikana kama Mapatano ya damu na vito vya thamani ( "blood for goods" deals )
Munk alihitimu katika Chuo Kikuu cha Toronto, Canada na kutunukiwa shahada ya electrical engineering mnamo Mwaka1952.

Mwaka 1958, Munk pamoja na wenzake walianzisha kampuni ya Clairtone kwa usaidizi David GilmourFrank Sobey. Baada ya hapo, amekuwa na mafanikio na changamoto nyingi katika biashara zake.

Amewahi kuwa Mhadhiri katika Chuo kikuu James Gillies Alumni Lecture, York University, Toronto. Amekuwa mjumbe katika bodi mbalimbali zikiwamo;


  • Trustee of the Toronto General Hospital.
  • Chairman of the University of Toronto Crown Foundation.
  • Member of the World Gold Council.


Pia Munk ni mjumbe wa heshima wa bodi ya taasisi ya Jewish National Fund (JNF) of Toronto, taasisi ambayo imekuwa na jukumu la kupora ardhi ya palestina na kuendeleza makazi ya Wayahudi kinyume na Azimio la Umoja wa Mataifa.

Taasisi hii ndio imekuwa kitovu cha ushirikino wa familia za Wahahudi wote ulimwenguni , ambapo moja ya jukumu lake kubwa ni kurudisha ardhi ya Israel iliyopotea kwa kuchangisha fedha na kununua ardhi kutoka kwa Palestine, kupanda miti, kujenga makazi na miundombinu mbalimbali.

Kutokana na uwezo, ushawishi na mafanikio yake, Munk amepata PHD za heshima katika Vyuo vikuu mbalimbali;


  • Doctorate from Upsala College, New Jersey.
  • Doctorate from Bishop's University, Quebec.
  • Doctorate from Concordia University, Montreal.
  • Doctorate from Technion – Israel Institute of Technology, Haifa, Israel
  • Doctor of Laws from Trinity College, University of Toronto,1995
  • Doctor of Sacred Letters from Trinity College, University of Toronto ,2004


Kutokana na tuzo hizo, Munk anatajwa kuwa afisa ambaye anaheshimika zaidi nchini Canada
Pia ni mwanzilishi wa Munk School of Global Affairs, kupitia mchano wa fedha kutoka taasisi yake ya Peter and Melanie Munk Foundation.

Chapisha Maoni

0 Maoni