
Abhay Chautala aliambia gazeti la Indian Express kwamba babake amekuwa kila siku akienda kusoma katika maktaba ya gereza hilo.Husoma magazeti na vitabu. Huwa anawaomba wafanyakazi wa jela kumtafutia vitabu avipendavyo zaidi. Husoma vitabu kuhusu wanasiasa maarufu duniani,2 amesema.Bw Chautala na 54 wengine, walipatikana na hatia ya kughushi vyeti walipokuwa wanwaajiri walimu 3,206 kati ya 1999 na 2000.Waendeshaji mashtaka walisema watu waliokuwa wamehitimu zaidi walikataliwa na badala yake wale waliokuwa wametoa hongo wakaajiriwa.
Bw Chautala ni kiongozi wa chama cha Indian National Lok Dal Party na ni mwana wa aliyekuwa naibu waziri mkuu Devi Lal.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA