Mnamo mwezi Julai 2017, Kampuni ya Progress rail Locomotives (PRL) ya Marekani ilileta vichwa vya treni 11 katika Bandari ya Dar es salaa kwa ajili ya kuviuza vyenye namba 9014, 9015, 9016, 9017, 9018, 9019, 9020, 9021, 9022, 9023 na 9024.
Tarehe 27 septemba, 2017 Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa aliteua kamati ya wataalamu kwa ajili kubaini kama vichwa hivyo ni vipya au la.Wajumbe wa kamati hiyo walitoka chuo kikuu cha Dar es salaam, TEMESA na shirika la Reli Tanzania (TRC).
Kamati hiyo ilifanya kazi hadi 15 oktoba, 2017 na kukabidhi ripoti kwa Mheshimiwa Waziri.Kamati ilibaini kuwa vichwa hivyo vya treni ni vipya.
Aidha tarehe 16 Oktoba, 2017 Mheshimiwa Waziri kwa mara nyingine aliteua kamati ya wataalamu wenye taaluma mbalimbali wakiwemo wanasheria wahandisi na wachumi kwa ajili ya kujadiliana bei ya kuvinunua vichwa hivyo.
Awali mwaka 2015,Serikali ilinunua vichwa kama hivyo 13 vyenye namba 9001, 9002, 9003 ,9004,9005,9006,9007,9008, 9009 ,9010, 9011, 9012 na 9013 kwa bei ya dola za kimarekani Milioni 3,200,000 kwa kichwa kimoja.
Kamati hivyo ilifanya majadiliano ya bei na kufikia muafaka wa kununua kwa dola za kimarekani milioni 2,400,000 kwa kichwa kimoja ambavyo ni pungufu ya dola 800,000 kwa kila kichwa cha treni kulinganisha na bei ya vichwa tulivyonunua awali,kwa maana hiyo kwa vichwa 11 serikali imeokoa dola 8,800,000.
Majaribio yatakuwa katika awamu tatu.Kwanza ni ukaguzi kwa kuvitizama(visual inspection),pili ni kuviwasha na kuvipa mizigo vikiwa havitembei(load box) na tatu ni kufunga na kuvuta mzigo tani 700 toka Dar es salaam hadi Morogoro na tani 1200 toka Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.
Ununuzi wa vichwa hivi 11 utaongeza ufanisi wa shirika kwani kwa sasa hivi tunavyo vichwa 29 madhubuti kati ya vichwa 47 tunavyovihitaji ili kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA