Wanawake Watatu Watiwa Mbaroni kwa Kutumia Jina la Rais Mstaafu Kikwete Kutapeli

Wanawake watatu waliofahamika kwa majina ya Mathe Uredi (41), Khadja Khamis (42) na Mwenge Uredi (33) wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kutumia jina la Rais mstaafu Jakaye Kikwete na familia yake kujipatia fedha kwa utapeli.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka hayo leo Machi 16, 2018 na kusema kuwa jeshi hilo limeweza kuwakamata watuhiwa hao ambao walikuwa wakitumia mtandao wa facebook kufanya utapeli kwa kutumia jina la Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete pamoja na Ridhiwani Kikwete.

"Wote walikamatwa wakiwa na simu za mkononi 12 zikiwa na line za mitandao mbalimbali na huku wakiwa na line zingine 10 zisizokuwa ndani ya simu line hizo ni za mitandao mbalimbali ambazo huzitumia ili kufanikisha uhalifu huo niliousema

"Watuhumiwa hao walifungua ukurasa huo wa facebook na wamekuwa wakitumia line hizo za simu kuwatumia na kuwapigia na kuwatumia message wananchi ili kuwashawishi kujiunga kwenye taasisi hizo na kisha kutumia line hizo kupokea miamala ya fedha kutoka kwa wakopaji wanaoweza kushawishika.
 
"Aidha watumuhiwa hawa wamekuwa wakiweka picha kwenye mtandao huo wa facebook wakionyesha watu waliobeba fedha kanakwamba watu hao wamenufaika kwa kupitia udanganyifu huo kwa kutumia majina makubwa na kuweka vitita hivyo viliwafanya watu kuamini kwamba kupitia vikoba hivyo wataendelea kujinufaisha na kupata mafanikio makubwa.

"Kwanza nitoe onyo kwa watu wote ambao wanaendelea kutumia majina ya viongozi waliiopo madarakani na waliostaafu kwa lengo binafsi ya kujinufaisha na kuchafua taswira ya viongozi na heshima zao basi jeshi la polisi halitamnyamazia mtu hata mmoja" alisisitiza Mambosasa

Watu hao watatu wanadaiwa kutumia mtandao wa facebook kwa kujiita Jakaya Kikwete Focus Vicoba, Salma Kikwete Focus Vicoba na Ridhiwani Kiwete Focus Vicoba na kuwatapeli wananchi fedha kwa njia za udanganyifu, Mambosasa amedai kuwa uchunguzi ukikamilika watawafikisha mahakamani watu hao.

Chapisha Maoni

0 Maoni