KAMANDA MANGU KUKANUSHA TAARIFA ZA WABUNGE JUU YA LUGUMI NA UFUNGAJI MASHINE

Mkuu wa Jeshi la Polisi – Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu amekanusha madai ya wabunge na hata taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kampuni ya Lugumi kushindwa kufunga mashine kwenye vituo vya Polisi 108 kama mkataba wake ulivyomtaka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, IGP Mangu alisema anashangazwa na habari hizo na kueleza kuwa kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mashine hizo kama ilivyokubaliana na serikali.

“Siyo kweli, watu wana ugomvi wao, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa intaneti,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.

Alipoulizwa mwenye jukumu la kufunga mtandao wa intaneti ni nani, IGP alijibu, “...ni TTCL (Kamuni ya Simu) ingawa sehemu nyingi ofisi zetu zimekatiwa huduma hiyo kwa kuwa jeshi halijalipa.”

Chapisha Maoni

0 Maoni