Kwa kawaida na hata biblia inasema, kusema uongo, kwa mfano, ni dhambi. Lakini je, kila uongo ni dhambi? Kuua ni dhambi, lakini je, kila unapoua unakuwa umetenda dhambi? Kuiba ni dhambi, lakini je, kila unapoiba ni dhambi? Maswali haya nimeyafanya kama sehemu ya mada yangu
ya leo, na zaidi kuyaeleza namaanisha nini, nimejikita sana kifalsafa, na tena falsafa rahisi kabisa.
Mara nyingi neno dhambi limekuwa likitumika karibu kila mahali na wakati mwingine neno hili limekuwa likiwafanya watu kutenda dhambi kwa kuamini kwamba wanachokitenda ni wema, kumbe yawezekana ndiyo dhambi hasa.
Mwanafalsafa mashuhuri nchini Ugiriki, Socrates aliwahi kudadafua kifalsafa akiamini kuwa, it is not good to call an act evil due to the fact that, every act is influenced by primacy of motive. Alitumia neno primacy of motive kwa maana ya kwamba, kila tendo analolitenda mtu huwa linasababu yake, kama sababu zingine, kwa hiyo ni nafsi yake peke yake ndiyo inayoweza kumhukumu aidha alichokifanya ni kizuri ama kibaya. Turudi katika maswali yetu ya awali hapo juu.
Uongo. Bila shaka hakuna kitabu cha dini kinachohararisha uongo: si biblia ama msahafu, kwa hiyo kiuhalisia kusema uongo ni dhambi. Swali la msingi hapa ni, dhambi hii inaitwa dhambi katika mazingira gani? Mfano, nikiulizwa kwamba, "...Hussein, umemuona Hassani akiiba?...". Ili kuepuka kutenda dhambi, nitasema NDIYO endapo kweli nilimuona kaiba, au HAPANA endapo sikumuona akiiba, nafikiri hapa nitakuwa nimeenda sawasawa na maandiko matakatifu. Lakini je, fikiria mfano huu. Ulikuwa unaishi Ujerumani kipindi cha chama cha Nazi* kikiwapiga na kuwaua wayahudi wengi. Nyumba ya mbele, karibu na unapoishi, kwa macho yako ukawaona wayahudi wamejificha kunusuri ama kujinusuru na mikono ya wanazi. Hata dakika mbili hazijaisha, ghafla mnazi anatokea na kukuuliza, bhana, umewaona wapi wayahudi? Hapo je, ungemjibu nini? Fikiria.
Hivyo, katika mazingira kama haya, Socrates aliamini, na hata mimi naamini kuwa, dhambi inahukumiwa nafsini mwa mtendaji mwenyewe, na si mwingine.
*ni chama chama kilichokuwa Ujerumani baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, chama ambacho kiliwachukia sana wayahudi kwa kuamini kuwa walikuwa wasaliti kwa kuiunga mkono serikali ya Weimar na kusaini mkataba wa amanai ulioandaliwa na League of Nations: mkataba ambao Hitler aliamini ni kandamizi kwa Ujerumani, na ulilenga kuinufaisha Marekani na washirika wake.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA