JE, WAJUA KUWA MOSUL NDIYO NINAWI YA YONAH? SOMA HAPA UPATE KUJUA.

Kama mnavyojua vita kali inaendelea huko Iraq kuwaondoa wahuni wa ISIS Mosul. Lakini jambo la kufurahisha nimekuja kugundua huu mji wa Mosul ndio hule Yona alitumwa Na Mungu kupeleka neno akala kona na kuingia chaka. Ikabidi atupwe baharin Na kumezwa Na nyangumi. Nadhan story mnahifaham.


Kumbe pia Ayubu ama Job alikuwa MuOmani ama Myemeni kaburi lake hadileo liko kati ya Yemen Na Oman.

Kumbe Pilato alikuwa Mfaransa (Gaul) ambalo lilikuwa jimbo la Kirumi.

Wale mamajus waliompelekea mwokoz wetu zawad walikuwa wakurd maeneo ya Tikrit Iraq.

Sodoma Na gomorrah ilikuwa ndio Syria.

Jezebel alikuwa mlebanoni (Phoenician) kutoka mji wa Sidon ambapo Sasa hivi Hezbollah wamejikita.

Mke wa musa Zipporah alikuwa Muafrika kutoka Ethiopia.

Nilikuwa najiuliza uislam ulifikaje hizi nchi Malasyia, Indonesia Na Brunei kumbe ni Otoman waturuki waliufikisha huko Ata mji wa Aceh ni kituruki.    

Chapisha Maoni

0 Maoni