Hitler alichukulia kama umoja kandamizi kwa Nchi adui wa Marekani, kama Ujerumani.
Kwa kipindi kirefu pia, rais Mugabe amekuwa akiukosoa sana umoja huu hasa kushindwa kutatua migogoro mikubwa kama ule wa Palestine na Israel ambao umedumu kwa miaka kadhaa sasa toka 1948 baada ya Israel (kihistoria) kuzaliwa. Pamoja na mengine mengi, rais Mugabe amekuwa akionesha ari ya kuwataka waafrika hata kujitoa uanachama wa Umoja wa Mataifa kwa kile ambacho amekuwa akikiita kuwa waafrika tumefanywa kuwa wajumbe wa muda wa Umoja huo. Hali kadhalika, Mugabe pia amekuwa akiutaka uongozi wa Umoja huu wa kimataifa kulifanyia marejeleo shirika la ulinzi la Umoja wa mataifa ili kulifanya liwe na wajibu sawia katika kusimamia usalama bila kujali mipaka ama vigezo vingine vya nchi.
Mugabe pia katika moja ya hotuba yake mjini Addis Ababa, alimtaka katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwatetea waafrika ili wapate haki sawa na mataifa mengine yanayojipa ukuu. Tujikumbushe hotuba hiyo ya rais Mugabe.
1 Maoni
Acha maoni yako ya nini kifanyike ili blog iendelee
JibuFutaTUANDIKIE MAONI YAKO HAPA