UPENDO PENEZA KUMTAKA RAIS JPM KUOONGOZA KWA MFANO NA KODI IKATWE KUTOKA KWENYE MSHAHARA WAKE



Upendo Peneza, mbunge wa viti maalum (CHADEMA) ametoa rai kwa rais Magufuli kuongoza kwa mfano na kumtaka naye akatwe
kodi ili aone uchungu wa kukatwa kodi na pengine atapunguza makato hayo hadi single digit kama alivyokuwa ameahidi na suala hilo kutotekeleza hadi sasa. Suala hilo limeibua sura mpya katika kujadili mpago wa maendeleo wa miaka mitano huku wabunge toka chama tawala wakimtaka kutokujadili suala la mshahara wa rais kwani ni kinyume cha sheria na kanuni za bunge.

Ameyasema na kuyathibitisha kwa dhati kabisa, ili kuwafanya wananchi wengine kulipa kodi kwa moyo mmoja, ipo haja rais JPM kuonesha mfano kwa kulipa kodi kutoka katika mshara wake.

"Mimi mbunge nalipwa mil 4, nakatwa kodi zaidi ya milioni moja...kodi pia ikatwe kutoka kwenye mshahara wake ili apate uchungu apunguze makato ya kodi hadi single  digit" Alisema Peneza.

Hoja kuhusu kukatwa kodi toka katika mshahara wa rais iliwahi kuzungumzwa na Tundu Lisu, mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma (CHADEMA).

Hii ni kutokana na ahadi ya rais juu ya punguzo la kodi hadi single digit kwa mishahara ya wafanya kazi, hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wengi bila mafanikio.

Chapisha Maoni

0 Maoni