MABADILIKO YA HALI YA HEWA: MTOTO GETRUDE ANENA UMOJA WA MATAIFA KWA NIABA YA WATOTO WENGINE.


Mtoto Getrude Clement kutoka Mwanza, Tanzania alipuka kwa kunena Umoja wa mataifa kwa niaba ya watoto wengine nchini Tanzania na kwingineko duniani. Alikaribishwa katika mkutano uliofanyika jijin Paris, Ufaransa: mkutano ambao uliibika na kutoa makubaliano ya pamoja yaliyokwenda kwa jina la Paris Agreement ambapo pia katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Ban Kin Moon alitumia fursa hiyo kwa ajili ya kusikiliza sauti za watoto ili kutoa ujumbe wao juu ya madhara ya madiliko ya tabianchi.

Mtoto Getruda alizungumza hayo kwa niaba ya watoto wengine na kutoa ujumbe huo katika mkutano huo huku akitoa wito kwamba, pamoja na kuwa walioko juu wanaweza kusema kwamba watoto hawawezi kujua madhara ya mabadiliko ya tabianchi
, lakini kiukweli ni kwamba, mabadiliko haya yataathiri zaidi watu walio katika tabaka la chini, na tabaka hili ambalo linajumuisha watu walio maskini ndilo litakaloathirika zaidi na mabadiliko haya.

Getruda alimaliza kwa kutoa wito pia kwa Umoja wa Mataifa kufikia muafaka ambao ungeweza kupambana sawia na mabadiliko hayo.

Chapisha Maoni

0 Maoni