Asimamishwa kazi kwa kukamata Wanyarwanda porini

 Kuna taarifa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mkuu wa Pori la Burigi mkoani Kagera, kwa kosa la mkuu huyo kukamata ng’ombe 400 walioingizwa na raia wa Tanzania na Rwanda porini humo.


Pamoja na mifugo, wenye ng’ombe hao wamekamatwa wakiwa na nyara (wanyamapori waliouawa).

Kusimamishwa kwake kumetokana na shinikizo la Wabunge wa Kamati ya Utalii, Maliasili na Mazingira wakiongozwa na Mbunge Musukuma, waliotaka mifugo hiyo iachiwe mara moja bila masharti.

Inaelezwa kuwa Mkuu wa Pori anayeitwa Bigilamungu, alihoji uhalali wa kuachiwa kwa ng’ombe pamoja na watuhumiwa hao waliokamatwa wakiwa na nyara za Serikali. Kitendo cha kusita kutekeleza amri hiyo, kumegharimu kazi yake!

Sasa wabunge wanashinikiza hata Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa naye asimamishwe kazi!

Chapisha Maoni

0 Maoni