IKULU: Tanzania na Morocco zasaini mikataba 22 katika sekta za Kilimo, Nishati na Mawasiliano.

Ziara ya Mfalme wa Morocco nchini Tanzania leo katika viunga vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwaajili ya shughuli mbalimbali za Kidiplomasia.

Tayari wageni mbali mbali wameanza kuwasili Ikulu Dar es Salaam akiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluh Hassan.


Waziri Mahiga: Uhusiano huu umeanza kipindi muafaka, mazungumzo yalianza katika sekta ya uchumi siku mbili zilizopita.

=======
Mwaziri wa Tanzania na Viongozi wa Morocco wametiliana mikataba ya maeneo ya ushirikiano katika sekta ya Kilimo, Mawasiliano, Nishati, Uvuvi ambapo jumla ya Mikataba iliyotiliwa saini ni 22.

Pia mataifa haya mawili wametiliana saini katika sekta nyingine za Bima, Mikopo, Benki ya BOA Tanzania LTD na hospitali ya CCBRT.

=====
Rais Magufuli: Urafiki baina ya TZ na Morocco ni wa siku nyingi, nawahakikishia wafanyabiashara wa Morocco mjisikie nyumbani.

Rais Magufuli: Nimehakikishiwa kutakuwa na ndege ya moja kwa moja kutoka Rabat Morocco hadi Dar es Salaam.

Rais Magufuli:
Niliipokuwa nikiongea na mtukufu mfalme nimemuomba atujengee msikiti hapa Dar es salaam na amesema ataujenga.

Rais Magufuli: Nimemuomba mtukufu Mfalme Mohamed VI atujengee uwanja wa mpira mkubwa Dodoma na amekubali ataujenga.

Rais Magufuli: Nilipokuwa nikizungumza na mfalme wa Morocco ameniomba kuongeza siku moja kukaa hapa na mimi nimemkubalia.

Rais Magufuli: Askari wetu watakwenda Morocco wiki ijayo kwa mafunzo ya kubadilishana uwezo.

Rais Magufuli: Mikataba hii 22 tuliyosaini leo ina lengo la kukuza ushirikiano wetu"

Rais Magufuli: Urafiki kati ya Tanzania na Morocco ni wa siku nyingi.    

Chapisha Maoni

0 Maoni