Lipumba: CHADEMA wameshindwa Kinondoni kwa sababu ya ubinafsi.

 Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba kasema kitendo cha CHADEMA kushindwa katika uchaguzi wa Umeya wa Kinondoni unatokana na ubinafsi mkubwa.

Lipumba kasema tokea awali alishauri mgombea wa umeya angetokana na chama cha CUF na sio CHEDEMA. "Kama sio ubinafsi na umangimeza wa rafiki zangu Chadema, upinzani tungeshinda hicho kiti" Lipumba

Lipumba kazidi kusema kuwa CUF ndio chama pekee kinachokubalika kwa Kinondoni. Na ndio maana hata mbunge wake ni wa CUF. Sasa hawa ndugu zangu wameleta ubinafsi mkubwa mpaka wameshindwa.

Mwenyekiti huyo kasema hayo katika ziara yake inayoendelea mkoa wa Dar es Salaam. Ambapo leo yupo kinondoni
 

Chapisha Maoni

0 Maoni