Picha!. Mfalme Mohammed III wa Morocco alivyotua Tanzania.




Mfalme wa Morocco Mohammed III amewasili jana nchini Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake rais Dr. Magufuli jijini Dar Es Salaam. Ujio huo wa mfalme umeambatana na msafara wa ndege tano na wajumbe zaidi ya 150 na vitanda na vifaa vingine muhimu kwa mfalme huyo.


Kama picha inavyoonesha, mfalme huyo akiambatana na mwenyeji wake amekagua gwaride lililoambatana na upigaji wa mizinga ipatayo 21 ikiwa ni ishara ya heshima kwa ujio wake.

Sanjari na hilo, ugeni huu unatarajiwa kuambatana na kusaini mikataba ipatayo 11 baina ya nchi hizi mbili.

Chapisha Maoni

0 Maoni