Vijitabia vya wanawake kutuashiria kuwa makini na kauli na matendo yetu.

Kama uko kwenye uhusiano na mwanamke halafu inatokea kila unachosema au unachomfanyia kinageuka kuwa kero kwake, juwa kwamba uko katika kipindi ambacho unapaswa kuwa makini sana katika mawasiliano yako na mwenzi wako.

Inatokea kwamba kila unalosema au kumwambia linapokelewa vibaya na kuzua mtafaruku kati yenu au kila unachojaribu kumfanyia kwa nia njema hupokelewa vibaya na kuzua maswali lukuki. Unajaribu kujiuliza maswali kwamba ni kitu gani kimemtokea mwenzi wako lakini hupati majibu, unapojaribhu kumdadisi unazua ugomvi.

Usijali huo ni upepo uvumao utapita na hali itakuwa shwari. Hapa chini nitaeleza sababu ya wanawake kuwa katika hali hiyo ili kuwa makini na kuchukua tahadhari wanapokumbana na changamoto hizo.

upload_2016-10-24_18-35-50.png
1. Wanapogombana na mashoga zao pika pakua.

Kwa kawaida mahusiano kati ya wanawake yanakuwa maji kupwa maji kujaa, kwa hiyo unaweza klukuta wanawake wameshibana na kuwa mashoga hasa wakishirikiana kwa kila jambo, lakini shetani akipita tu urafiki wao unaweza kuingia msukosuko wakagombana kiasi cha kushangaza. Kama mwezi wako akigombana na shogake kuwa makini, akili yake inakuwa na kuchanganyikiwa kwingi. Mnajua kwa nini, kuna mambo mengi waliwahi kushirikishana yakiwemo ya siri, hapo anakuwa na wasiwasi kwamba huenda siri zake zikavuja na ile kuvunjika kwa urafiki wao kunamfanya kuishi kwa wasiwasi
2. Wakigombana na mama zao

Mtoto kwa mama hakui na wazazi mara nyingi hujiona wana mamlaka kwa watoto wao hata kama ni wakubwa. pale mwanamke anapokuwa na mji wake anajiona ana mamlaka yake na maamuzi wake, ikitokea mama akianza kumpangia jambo la kufanya katika mji wake hukasirika sana na kuhisi kuingiliwa katika mji wake. Kama ikitokea mwezi wako akigombana na mama yake usitarajie akawa na hali yake ya kawaida. jambo hilo litamchanganya sana na huenda hata nyumbani kwake pia kusiwe salama. kwa hiyo kuwa makini pale unapowasiliana naye na kamwe usionekana kumsema kwamba amekosea bora kukaa kimya. ndugu wakigombana chukua jembe ukalime. labda kama akigundua kwamba ni yeye mwenye tatizo na anahitaji msaada wako ili kumsuluhisha na mama yake

upload_2016-10-24_18-45-15.png

3. Wakiwa kwenye siku zao

Kuna baadhi ya wanaume bado zile mood za kupata hedhi kwa wenzi wao hawajazikariri na hivyo kushindwa kujiandaa kisaikolojia kukubaliana na visirani vya wenzi wao wakiwa katika siku zao. Kuna baadhi ya wanawake kimaumbile huwa katika mood wiki moja kabla au wakati wa hedhi au baada na wengine huweza kubebe visirani kwa wiki mbili yaani kipindi cha kabla na hata baada ya hedhi. Wanaume wanatakiwa kuwa na kumbukumbu ili wasishangazwe na mabadiliko ya kitabia ya wenzi wao

upload_2016-10-24_18-51-5.png

4. Wakidhalilishwa kazini

Kuna wakati huko makazini maboss huwa na siku mbaya na kuhamishia hasira zao kwa watumishi wa chini. kama mkeo kakutana na kisirani cha boss wake jiandae kubeba sehemu ya kisirani hicho.
upload_2016-10-24_18-53-15.png

5. Kama hawakualikwa kwenye sherehe na mtu wao wa karibu

Kama mwenzi wako hakualikwa kwenye sherehe ya aina yoyote, iwe ni wedding anniversary, Birthday Party nk. Jua kwamba jambo hilo litamkera sana na kumuacha na maswali mengi sana kichwani kisi cha kumvuruga kichwa. Kuwa makini sana wakati wa kuongea naye unaweza kujuta.

upload_2016-10-24_18-57-23.png

6. Ole wako usahau birthday yake

Utajuta nawaambia. usije ukajifanya unajipendekeza baada ya kuwa umesahau mpaka akafanyiwa birthday na mashoga zake we huna habari utajuta

upload_2016-10-24_18-59-27.png

7. Wakiwa na msongo wa mawazo na sononi.

Wape muda mpaka watulie ndipo unaweza kuuliza kwa upole, kama hawako tayari piga kimya. wanawake siyo watu wa mchezo mchezo...
 

Chapisha Maoni

0 Maoni