Polisi wanne wametiwa mbaroni mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumvua
nguo mchungaji mmoja na kumpiga picha za utupu na mtu mwingine ili
wamtuhumu kwamba anafanya mapenzi ya jinsia moja Katika mkasa huo uliotokea ndani ya chumba cha hoteli moja wilayani Hai, polisi hao wanadaiwa kumpiga picha na kisha kumtaka atoe shilingi 10 milioni ili kumaliza suala hilo, alitoa shilingi 5 milioni na kuachiwa huru
Habari za uhakika zilizofikia gazeti hili jana, zinasema tukio hilo limetokea Jumatano iliyopita kati ya saa 10 alasiri hadi saa tatu usiku huko Bamang'ombe
Katika tukio hilo linaaminika kuwa lilitengenezwa na polisi hao kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa mchungaji huyo ambaye jina lake na kanisa analohudumu tunalihifadhi kwa sasa, baada ya kukutwa wawili hao ndani ya chumba, waliwaamuru wavue nguo wakiwatuhumu kufanya mapenzi ya jinsia moja na kuwapiga picha kwa kutumia simu zao

0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA