Ajali: Ndege yaanguka na kuua waliokuwemo wote huko Indonesia



 NDEGE ye jeshi la anga ya Indonesia aina ya Hercules C-130 imeanguka katika eneo la misitu nchini Papua na kuua watu wote waliokuwemo ndani yake ambao ni marubani watatu na wanajeshi 10.
Mnadhimu wa jeshi, Agus Supriatna aliiambia shirikala habari la Metro TV kwamba huenda hali ya hewa ndiyo iliyosababisha ajali hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa imebeba chakula kutoka Timika kwenda Wamena ilipoanguka milimani karibu na sehemu iliyokuwa inakwenda.

Chapisha Maoni

0 Maoni