Baada ya mchumba kugoma, Pendo wa maisha plus atamani ndoa

MSHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus Season 11 aliye pia msanii wa filamu za Kibongo, Upendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’ amefunguka kuwa kwa sasa anatamani sana kuingia katika maisha ya ndoa licha ya mchumba wake kuchelewa kuchukua uamuzi huo.

Upendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Leaders Club jijini Dar, Pendo ambaye alionesha kipaji cha juu katika uigizaji ndani ya filamu za Devils Kingdom na Moses za marehemu Steven Kanumba, alisema amechoka kuishi maisha ya peke yake kwani heshima ya mwanamke mwenye umri kama wake ni ndoa.
Aidha, aliongeza kuwa mwanamke akiolewa huweza kujiepusha na mambo mengi mabaya ikiwemo starehe zisizokuwa na msingi kwani maisha ya ndoa hubana na kumtuliza mwanamke.

Chapisha Maoni

0 Maoni