Bamper to bamper, Mwana FA ajiandaa kuachia kitu kingine kipyaaa!!


Hit Maker wa “Dume Suruali” Mwana FA, ni mmoja kati ya wasanii wanaofunga mwaka vizuri kwenye tasnia ya muziki hapa Tanzania, kwani Single yake hiyo ni moja ya ngoma zinazofanya vizuri kwenye Media, Club na Mtaani pia.




Mwana FA
Dume Suruali mpaka sasa bado ni gumzo kutokana na ujumbe uliopo ambao wanaume/wanawake wengi huutumia kufikisha ujumbe kwa watu wao wawapendao.
Sasa hata kabla ya wimbo huo kusahaulika masikioni mwetu, Mwana FA anaandaa Jiwe lingine tena ambalo hata hivyo naamini litakuwa ni hit kwani hajawahi kuwaangusha mashabiki wake tangia enzi zile za Nina Mabinti Damu Damu mpaka leo hii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram FA kapost picha (hapo juu) ikiwa imeandikiwa caption hii “another one…” akimaanisha kuna ngoma mpya inakuja ingawaje bado hajaweka wazi wimbo huo unaitwaje? amemshirikisha nani? na utatoka lini? 

Chapisha Maoni

0 Maoni