Boko Haram watimuliwa msitu wa Sambisa

Wanajeshi wa Nigeria
Wanajeshi wa Nigeria
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, anasema jeshi limeiteka kambi muhimu ya wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram iliyo msitu wa Sambisa.

Alisema kambi hiyo katika Msitu wa Sambisa, kaskazini-mashariki mwa nchi, ilitekwa siku mbili zilizopita.
Rais Buhari alisema Boko Haram sasa haina pahala pa kujificha, baada ya kutimuliwa kutoka maficho yake makubwa.
Katika miezi ya karibuni, jeshi limekomboa maeneo mengi yaliyo-dhibitiwa na wapiganaji hao; lakini bado wanafanya mashambulio ya kujitolea mhanga katika nchi jirani za Niger na Cameroon.
Kumekuwa na uvumi kuwa baadhi wa wasichana wa Chikob ambao walitekwa nyara mwaka 2014 wanazuiliwa ndani ya msitu huo.
Baadhi ya wasichana waliofanikiwa kukimbia muda mfupi baada ya kutekwa nyara wanasema kuwa walikuwa wakishikiliwa eneo hilo.
Jeshi limetwaa maeneo kadha ambayo awali yalikuwa yakidhibitiwa na Boko Haram tangu harakati za kulishinda kundi hilo zianze.
Inaaminika kuwa baadhi ya wasichana waliotekwa walishikiliwa eneo hilo
Inaaminika kuwa baadhi ya wasichana waliotekwa walishikiliwa eneo hilo.BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni