CCM yatoa tamko hofu ya mabadiliko ndani ya chama

 Chama cha Mapinduzi CCM kimetetea uamuzi wake wa mabadiliko ya kimuundo na uendeshaji wa chama hicho na kukanusha hisia za baadhi ya watu kuwa mabadiliko hayo yamezua hofu ndani ya chama.


Taarifa iliyotolewa leo kupitia kwa Katibu wa Katibu Mkuu wa CCM, bwana Charles Charles imeeleza kuwa mabadiliko hayo yamepokewa kwa shangwe ndani na wanachama wote wa chama hicho na wala hayamlengi mtu yoyote ndani ya chama.

Kuhusu ya kupunguza Wajumbe wa Kamati Kuu kutoka 34 na kubaki 24 na Wajumbe wa NEC kutoka 388 na kubaki 158, taarifa hiyo imesema imesema kuwa tangu kutangazwa kwa mabadiliko hayo siku ya Jumanne Desemba 13, 2016 hakuna mwanachama, kiongozi wala mfuasi yeyote wa CCM aliyelalamika, kuhoji au kunung'unukia mabadiliko yoyote yaliyopitishwa na vikao hivyo.

Taarifa hiyo ikitetea zaidi maamuzi hayo imesema “Kama watu watano wanaweza kuwawakilisha wana CCM wote katika mkoa mzima kwa mfano, inawezekanaje kwa wawakilishi 158 kwa mikoa 31 waonekane wachache? Lakini pia, hivi watu 388 wanapokutana mahali hicho kinakuwa kikao au mkutano wa hadhara ambao hata mijadala yake inaweza isifanyike kwa usahihi? Hivi inawezekana kwa watu wote hao kuchangia kwenye kikao cha siku moja au mbili tu?”

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na viongozi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma mara baada ya kukabidhiwa ofisi.

Pia, kuhusu kuondolewa kwa nafasi kadhaa za ujumbe wa NEC chama hicho kimesema hakuna uhusiano wowote ule na madai ya rushwa ila ni mageuzi ya kawaida ndani ya chama.

“Ni mageuzi ya kawaida ambayo yamekuwa yakifanyika kwa kuletwa au kuletwa tangu wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne hadi hii ya tano, hivyo hakuna uhusiano wowote na kulengwa mtu yeyote ila ni kutaka kukidhi malengo ya kisiasa kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa duniani kote”


Chapisha Maoni

0 Maoni