Real Madrid yanyakua ubingwa kombe la club bingwa duniani

 Klabu ya Real Madrid siku ya jumapili ya December 18, ilicheza dhidi ya Kashima Antlers ya Japani kwenye fainali ya FIFA Club World Cup.


Real ilipata goli lake la kwanza kunako dakika ya tisa kupitia mshambuliaji Karim Benzema, lakini Gaku Shibasaki alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili na kuiweka mbele Kashima.

Hadi dakika ya 90 mchezo uliisha kwa matokeo kuwa ni 2-2.

Mechi ikaelekea kwenye dakika za nyongeza na hapo ndipo Ronaldo akaamua mechi hiyo kwa kufunga hat-trick.

Baada ya filimbi ya mwisho Madrid ikawa mshindi kwa magoli 4-2.

Ushindi huo unaipatia Real Madrid kombe la pili la klabu bingwa dunia na kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa katika mechi zote hadi mechi 37.

Hatua hiyo ina maana kwamba washindi 10 wa taji hilo wanatoka bara Ulaya.

Chapisha Maoni

0 Maoni