LIGI KUU BARA: Mkude akaribia kutua Yanga

Kudai haki yake ya msingi kumesababisha mchango wake ndani ya timu kutothaminika na kutishiwa kutemwa mwishoni mwa msimu huu
Klabu ya Simba ipo kwenye mpango wa kusajili mbadala wa nahodha wao Jonas Mkude, baada ya mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya huku akiutolea maneno ya hovyo viongozi wake.

<<<DOWNLOAD MAHENGA BLOG APP HAPA>>>

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe ameiambia Goal, wamechoshwa na maneno ya mchezaji huyo na sasa wanaona nivyema wakamtafuta mchezaji mwingine ambaye atamudu kwenye nafasi hiyo.

“Tumeanza mipango ya kutafuta mchezaji mwenye uwezo zaidi ya Mkude, wa nafasi ya kiungo mkabaji kwasababu mchezaji huyo amekuwa na maneno mengi kuliko mchango wake kwenye timu,”amesema Hans Poppe.

Kiongozi huyo amesema mchezaji Mkude anataka kupewa dau kubwa kama ilivyo kwa wachezaji wa kimataifa, lakini kiwango chake ni chakawaida hivyo wanaona nivyema wafanye maamuzi mapema katika kipindi hiki cha dirisha dogo.

Amesema hadi sasa hakuna mchezaji waliyemlenga lakini wamepanga kumtafuta mchezaji huyo kwenye mataifa ya nje kwakua wanataka mtu mwenye uwezo tofauti kwa ajili ya kuifikisha mbali timu yao hasa ukizingatia wanamatarajio ya kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa siku zijazo.

“Mkude ni mchezaji ambaye tumemkuza wenyewe na tumekabidhi majuku, lakini anajifanya amekuwa na wakati hata asipokuwepo kwenye timu hatupati madhara yoyote,”amesema Hans Poppe.

Yanga yamtema rasmi Mbuyu Twite

Katika siku za karibuni Mkude, aligoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Simb, baada ya viongozi wa timu hiyo kumpa kiasi kidogo cha pesa na yeye kutaka kupewa dau la milioni 80 badala ya 50 wanazotaka wao.

Baada ya uongozi kugoma kutoa kiasi hicho cha pesa Mkude amesema ataondoka na kujiunga na mahasimu wao Yanga baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu.

Mkude amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba, na amecheza mechi zote za mzunguko wa kwanza wa ligi ya Vodacom Tanzania na kuifaya timu hiyo kumaliza nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 35.

Chapisha Maoni

0 Maoni