Makala maalumu: Sanda Iliyotumika Kumzika Yesu Inategua Kitendawili cha Sura Yake Halisi?

kwa kuwa watu wengi wametia mikono kuandika mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, kama walivyohadithiwa wale waliokuwa mashahidi kuyaona......... nimeona ni vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa hayo mambo tangu mwanzo, kukuandikia taratibu............. upate kujua uhakika wa mambo yale uliyofundishwa..."

Luka 1: 1 - 4.

Wakuu, nikiwa namalizia kuandika makala ambayo karibuni naiweka hapa.. Nimepata ombi maalumu kutoka kwa Mkuujisanja kuwa niandike kiasi kuhusu Cesare Georgia. (Mkuu jisanja ameandika pia uzi kuuliza habari za huyu mtu Naomba kujua kuhusu CESARE BORGIA )
Sasa huyu jamaa historia yake ni ndefu mno ila nimeona ni vyema labda niongee kidogo kijipande kidogo ambacho labda ndicho kimeleta impact kubwa zaidi mpaka katika nyakati hizi tunazoishi sisi..

Cesare Borgia na Sura ya Yesu.

Cesare Borgia alikuwa ni mtoto wa nje wa Papa Alexander VI (1492 - 1503) ambaye alizaa na hawara yake aliyeitwa Vanozzza dei Catanei.

Baada ya Borgia kufikia umri wa miaka 18 baba yake Papa Alexander VI alimfanya kuwa moja ya makadinali katika eneo la Italia ambalo lilikuwa chini ya utawala wa Papa.

Baadae Borgia alikuja kukumbwa na kashfa kubwa ya kumuua kaka yake aliyeitwa Giovanni kutokana na wivu. Moja, Borgia alisikia wivu kwasababu kaka yake alipandishwa cheo kuwa Jemedari wa majeshi ya Papa lakini pili ulikuwa ni wivu wa mapenzi kwani wote wawili walikuwa wanajihusisha kimapenzi na mke wa mdogo wao aliyeitwa Giofre.
Kashfa hii ilichangia kumfanya Borgia kuingia katika historia ya kuwa Kadinali wa kwanza kujiuzuru wadhifa huo.

Baadae mfalme wa Ufaransa Louis XII alimfanya Borgia kuwa mtawala wa eneo la Valentinois na hii ndio ilikuja kupelekea kuitwa jina la utani la 'valentino'.

Katika historia iliyoandikwa kwenye kitabu chaTriptych of Poisoners. Inaeleza kwamba mwaka 1503 Borgia alimuajiri Leonardo da Vinci kuwa muhandisi katika jeshi lake. Katika kipindi hiki pia Leonardo pia alikuwa anaendela na kazi zake za uchoraji.

Kuna habari zinaeleza kwamba kuna uwezekano kuwa Leonardo na Borgia waliingia katika uhusiano wa mapenzi na hii inadhihirishwa zaidi na 'obsession' ya Leonardo juu ya Borgia.

Katika picha zote ambazo leonardo alichora kuhusu Masihi Yesu Kristo alipofika hatua ya kuchora uso, alichora sura ya Borgia.
Kutotokana na umaarufu wa Leonardo na ushawishi ambao Borgia alikuwa nao Vatican, ilikuja kukubaliwa kwa picha mojawapo ya picha za Yesu (yenye sura ya Borgia) ikawekwa ndani ya kasri la Papa.

[​IMG]
Cesare Borgia

[​IMG]
Mfano wa picha ya Yesu iliyochorwa na Leonardo da Vinci ikiwa na sura ya Borgia

Kitendo hiki cha 'Picha ya Yesu' kuwepo ndani ya Kasri la Papa ndicho kilichangia kuenea kwa sura ya Borgia kukubalika kuwa ni sura ya Yesu.

Hata ilipofika karne ya 20 na walipotokea watu wanatengeneza Filamu kuhusu maisha ya Yesu alitafutwa mtu ambaye anafanana na sura ya Yesu inayokubalika na kuaminiwa na wengi (Sura ya Borgia).

Kwahiyo kwa maneno mengine hii 'Sura ya Yesu' tuliyonayo vichwani mwetu ni Sura ya Borgia ambayo iliigizwa na Brian Deacon.
Ndio kusema Brian Deacon alipata nafasi ya kuigiza kwa kuwa ndiye muigizaji ambaye sura yake inarandana na Cesare Borgia.

Je, Sanda ya maziko ya Yesu (Shroud of Turin) inatengua kitendawili cha 'Sura halisi ya Yesu'?

[​IMG]

Kuna kitambaa kirefu kimehifadhiwa katika Kanisa maarufu la 'Cathedral of Saint John The Baptist' nchini Italia katika mji wa Turin. Kitambaa hiki kinaaminiwa na wengi kuwa ni sanda aliyozikiwa Masihi Yesu Kristo mara baada ya mwili wake kuondolewa msalabani.

Historia inaonyesha kwamba kitambaa hiki kilianza kuongelewa katika nyanja za kidini/imani miaka ya 1390.

Madaktari wa kujitegemea wa Forensic waliokipima kitambaa hiki wametoa conclusion kwamba kitambaa hicho kinaonyesha kuwa kilifunikwa kwa mtu aliyekuwa na urefu kati ya futi 5 na inch 7 mpaka futi 6 na inch 2.

Pia aliyefunikwa kitambaa hiki madaktari wamedhihirisha kwamba mtu huyo alikuwa na majeraha makubwa viganjani, na miguuni (misumari ya kuangikwa msalabani). Pia alikuwa na majeraha kwenye paji la uso (Taji la miba), michirizi ya damu mikononi na jeraha kubwa ubavuni (Yesu alichomwa mkuki ubavuni akiwa msalabani yakatoka maji na damu).

Pia kitambaa hiki ina sura ambayo haionekani kwa macho ya kawaida na haikuwahi kujulikana kama ina picha isiyoonekana kwa macho mpaka pale miaka ya karibuni walipopiga picha ya 'negative' ya kitambaa hiki ikajitokeza sura ya mwanaume mwenye nywele ndefu, ndevu na mustachi. (Tazama picha chini).

[​IMG]
Picha ya negative ikionyesha sura ndani ya should of turin.

Kuna utata mkubwa kuhusu kitambaa/sanda hii.. Kwani pia wanasayansi walitumia teknolojia ya Carbon 14 kupima umri wa kitambaa hiki na kugundua kwamba kilitengenezwa (kilianza kuexist) miaka 800 tu iliyopita (1200's).

Kwahiyo watu wanaopinga kuwa hii si sanda ya Yesu hii ni moja ya hoja zao kuu kuwa kama kweli ilikuwa ni sanda ya Yesu Carbon 14 ilipaswa kuonyesha kina miaka si chini ya 2000.

Lakini wanaotetea kuwa hii ni sanda ya Yesu wanadai kuwa ni impossible kutengeneza kitu cha kugushi cha kiwango hiki.

Kwa mfano sura kwenye kitambaa hiki inaonekana pekee ukitumia vyombo vya teknolojia vinavyotoa picha ya 'negative' hii inamaanisha image imejipandikiza ndani ya kitambaa (sio juu au nyuma).

Wako wanasayansi wanaosema kuwa ili utengeneze kitu cha kugushi cha kiwango hiki unapaswa kutumia mionzi maalumu (atomic laser) teknolojia ambayo haikuwepo kipindi hicho cha miaka ya 1200's.

Mjadala kuhusu 'sanda ya Yesu' ni mkali mno.
Kanisa katoliki halijawahi kuikataa au kuikubali rasmi kama hii ni sanda halisi ya Yesu.

Lakini mwaka 1958 Papa Pius XII aliikubali Sura iliyoonekana kwenye kitambaa hiki kuwa ndiyo Sura halisi ya Yesu. Na Papa John Paul II amewahi kutamka kuwa kitambaa hiki 'Shroud of Turin' kinaakisi injili/kioo cha injili ("a mirror of the gospel)

[​IMG]
Papa Francis alipotembelea eneo la hifadhi ya Should of Turin

Chapisha Maoni

0 Maoni