Mwinyi: Waislamu walikuwa wakilazimishwa kula nyama ya nguruwe kidogo ilete ugomvi mkubwa

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi amedai kulikuwa na manunguniko makubwa yaliyokaribia kuleta ugomvi Tanganyika kati ya waislam na wakristo kutokana na waislamu kulazimishwa kula nyama ya nguruwe, alitoka Zanzibar kuja kusuluhisha ugomvi huo na kuweka uhuru kila mtu ale chochote anachokitaka ndio sababu kubwa ilisababisha akaitwa mzee ruksa.


Pia aliruhusu biashara ya nchi hii iwe ruksa vilevile ikawa inaendeshwa na mashirika binafsi na sio mashirika ya umma tu.

Amesema pia sasa hivi kuna hakuna umoja na watu wanatengana kutokana na kuwa na itikadi tofauti za kisiasa.


Chapisha Maoni

0 Maoni